NEWS

18 Aprili 2014

Tiwa Savage ajipunguza na kutengeneza muonekano mzuri kwenye ndoa yake ya kisasa

Mwimbaji wa Nigeria, Tiwa Savage nae anatarajia kufunga ndoa ya kisasa (kizungu) April 26, huko Dubai baada ya kufunga ndoa ya kimila November mwaka jana na ameripotiwa kuupunguza mwili wake ili awe na muonekano mzuri siku hiyo ya tukio.



Hata hivyo, haijulikani kama mwimbaji huyo wa Nigeria anaefanya kazi chini ya Mavin Records amefanya uamuzi wa kulala na kivazi maalum kama Kim Kardashian au anatumia njia ya kawaida ya kupanga ‘msosi’ na kufanya mazoezi.

Tiwa ameolewa na meneja wake Tunji ‘Tee Billz’ Balogun.