Beyonce ni miongoni mwa wanawake walioingia katika orodha hiyo ya Forbes akiwa ameshika nafasi ya 17. Wanawake wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Hillary Clinton katika nafasi ya 6, Michelle Obama no.8 na Oprah Winfrey amekamata no 14.
Wanawake wengine maarufu waliotajwa ni Angelina Jolie kwenye nafasi ya 50, Mcolombia mwimbaji Shakira katika nafasi ya 58, Lady Gaga amekamata nafasi ya 67.

