VEVO ni mtandao wa internet unaoshughulika na video za muziki na wanamuziki unaomilikiwa na kampuni kubwa za muziki duniani SONY Music Group, Universal Music Group, Warner Music Group na Google. VEVO ni mtandao number moja duniani unahusika na kuhifadhi na kurusha kazi za muziki za wanamuziki maarafu duniani, kama Jay Z, D’banji, Nick Minaji, Mafikizolo na wengine wengi.
Video ya Gosby Iliyoingia kwenye Vevo
Akizungumzia juu ya kupata Account hiyo ya VEVO, Gosby amesema: Nina furaha kubwa sana kwa kuwa mara nyingi nimekuwa natamani kuwa na account ya VEVO. VEVO ni platform kubwa ya wasanii na wadau wa muziki duniani, nafurahi kuwa miongoni mwao sina shaka kazi zangu zitatazamwa na wadau wakubwa wa soko la muziki Afrika na dunia. Yeah unaweza kuwa na video zako YouTube kama wanamuziki wengine au hata wasio wanamuziki lakini VEVO ni maalum kwa Established Musicians Only, hata mtu akitazama Music Video zako VEVO anakuwa na uhakika wa kuwa hii ni video ya established artist Nadhani ni njia iliyo sahihi kwa wanamuziki wa kizazi kipya hapa nyumbani kujaribu kupata VEVO accounts, wenzetu wa Afrika Magharibi na Afrika Kusini wanamuziki wao wote wakubwa wana VEVO accounts, mapinduzi yetu ya muziki yasiishie kwenye platform za hapa nyumbani tu, ila tutumie fursa zaidi za masoko na kujitangaza kwenye mitandao mikubwa duniani ili kuwa na wigo mpana zaidi wa kutangaza kazi zetu na nchi yetu,” amesema.
“Imeichukua management yangu takribani mwezi mmoja na zaidi kufuatilia, kujaza ma form na finally kuwa accepted na VEVO inayopatikana kwenye Youtube.com na VEVO.COM. Nichukue fursa hii kuipongeza management yangu kwa kazi nyingine bora na yakujivunia na vile vile nitumie fursa hii kuwapongeza mashabiki wangu kwa uvumilivu waliokuwa nao katika kipindi hiki cha ku-migrate kazi zangu kutoka youtube na kwenda VEVO , video yangu ya BMS ilikuwa na Views 45,000 kipindi tunaishusha ili kuweza kuhamia VEVO ikiwa ni moja ya masharti ya VEVO ili kuzuia duplication.”
Mbali na suala la VEVO, Gosby ameongelea wimbo wake mpya anaotarajia kuutoa hivi karibuni aliomshirikisha Ommy Dimpoz na nini kitarajiwe kutoka kwake mwaka huu.
“Yeah nina kazi nyingi ambazo ziko kwenye studio tofauti tofauti na ambazo nimefanya na producers tofauti tofauti kama 10 hivi na zimefanywa na producers tofauti kama 7 wa hapa nchini na nje ya nchi, lengo ni kuleta ladha tofauti ya muziki na kujifunza kuhimili pressure ya kufanya kazi na watu tofauti tofauti. Kwa muda wa miezi miwili nimekuwa nashauriana na management yangu na baadhi ya wadau wa muziki ili kuona ni wimbo gani tuutoe kwanza na lini kwa kuwa nina nyimbo nyingi nzuri na zilizotofauti sana na mwisho tumeamua tuachie wimbo niliomshirikisha Ommy Dimpoz unaoitwa NAOGOPA. Sababu ya kupendekeza wimbo huo ni kutokana na aina ya muziki wenyewe, na wakati wa sasa. Katika wimbo huu mimi na Dimpoz tumejaribu kulalamikia changamoto tunazokutana nazo kutokana na wapenzi tunaokutana nao lakini mwisho wa siku tunaendelea kuwa nao, na ninadhani ni kitu ambacho huwakuta wengi, wimbo utatoka hivi karibuni. Kitu kingine ni mjiandae na video zenye ubora zaidi baada ya video yangu ya BMS kuanza kuchezwa na TV za nje ikiwamo Channel O na kuvuna mashabiki wengi wa nje , imetupa faraja na ari ya kuongeza uwekezaji zaidi kwenye video, so mjiandae kwa ngoma kali na video kali.”