NEWS

1 Mei 2014

Kanisa katoliki lakanusha ripoti kuwa msemaji wa Vatican alisema ‘Hakuna dalili za Yesu kurudi’

Kanisa katoliki limedai kuwa habari za ‘anayedaiwa kuwa’ msemaji wa Vatican, Kardinali Salvatore de Giorgi kwamba hakuna dalili za Yesu kurudi si za kweli na hakuna kardinali mwenye jina kama hilo.


Katika habari hiyo iliyosambaa mtandaoni, Kardinali Giorgio Salvadore anadaiwa kutangaza rasmi kuwa huu ni mwaka wa 1,981 na wa mwisho wa Vatican waliouweka kumsubiri Yesu kurudi tena duniani na kwamba hata hivyo amewataka waumini kuendelea kuwa na imani licha ya habari hiyo. Kardinali Salvadore anadaiwa kusema: Tunahisi Yesu haji tena kwa jinsi inavyoonekana. Ni miaka mingi. Huenda akawa amebanwa akifanya mambo mengine mazuri kwa watu sehemu nyingine.”
Katika sehemu mbalimbali za biblia kikiwemo kitabu cha Yohana, 14:1-3, Yesu aliwaahidi mitume wake kuwa atarehea tena. “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo.”
Kwa mujibu wa Askofu Joseph Osei-Bonsu wa nchini Ghana, amesema kauli hiyo inayodaiwa kusemwa na msemaji Vatican sio kweli.
‘Hakuna kardinali yeyote kati 216 wa kanisa katoliki mwenye jina la Cardinal Giorgio Salvadore,’ alisema. ‘Kweli yupo Cardinal Salvatore de Giorgi, Archbishop Emeritus wa Palermo. Majina hayo mawili hayafanani, na pia Cardinal Salvatore de Giorgi ni Askofu aliyestaafu na sio msemaji Vatican,’ Osei- Bonsu alielezea.
Alisema msemaji mkuu wa Vatican anaitwa Fr. Federico Lombardi.