NEWS

3 Mei 2014

Mfungwa awashitaki Jay Z, Beyonce, Kanye West, Chris Brown na Rihanna, adai walimuibia nyimbo 3,000 akiwa gerezani

Katika hali isiyo ya kawaida, polisi wa California wamepokea mashitaka toka kwa mfungwa mmoja akiwashitaka wanamuziki wakubwa wa hip hop, na R&B akiwadai fidia ya $ bilioni 2.



Katika faili la kesi hiyo, mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Richard Dupree amewataja Beyonce, Jay Z, Kanye West, Rihanna na Chris Brown kuwa walimuibia mashairi ya nyimbo zake 3,000 alizoandika wakati akiwa gerezani.

Kwa mujibu wa huffingtonpost, Dupree alifungua mashitaka katika mahakama ya wilaya ya mashariki mwa California April 21, na anaamini kuwa Beyonce na Jay Z walifanya kazi na CIA, FBI na vitengo vingine vya ulinzi wa Marekani kumpeleleza na kuyapata mashairi yake..

Anaamini kuwa Chris Brown, Kanye West na Rihanna walihusika na ku-organize kundi la watu waliomuibia mashairi ya nyimbo hizo 3,000.

Habari hii ya kweli inaweza kuchukuliwa kama sehemu ya ucheshi kwa wote waliotajwa lakini Dupree yuko serious.

Bofya hapa kusoma shauri lilofikishwa mahakamani hapo.