Lakini Mez B ni mfuasi mzuri wa vitendo wa kauli ya Ben Pol ‘Jikubali’ na anaamini kuwa yeye ndiye mkali zaidi ya wakali wote ambao ungeweza kuwafikiria incase aumfikirii yeye.
Member huyo wa Chamber Squad, alisema kuwa yeye anaamini kabisa kuwa ndiye msanii anaeimba kuliko wasanii wote Tanzania na kwamba inawezakana ikawa hata kwa Afrika Mashariki.
Mez B ambaye hivi karibuni ameachia wimbo mpya unaitwa ‘Shemeji’ amefunguka baada ya kuulizwa kuhusu alivyojipanga kurudi kwenye game na kupenya katikati ya wasanii wapya wenye vipaji vya hali ya juu.
“Mimi kwanza nawapongeza wasanii wote kwa sababu wana vipaji vizuri, ni changamoto nzuri. Kwa mimi Mez B na kwa mtu anaemfuatilia Mez B, Mez B ni msanii mwenye kipaji cha kipekee sana, sijifananishi na msanii yeyote Tanzania. Sisemi hivyo kama watu hawafanyi vizuri…watu wanafanya vizuri. Lakini mimi naamini naimba kuliko msanii yeyote Tanzania. Labda hata Afrika Mashariki.” Amesema Mez B.
Mwimbaji huyo ameeleza kuwa anaamini angeonekana zaidi kama kiwanda cha muziki Tanzania kingekuwa tofauti na kilivyo sasa.
“Kama game ingekuwa linaruhusu tufanye kweli muziki international, sio huu muziki ambao wanahip hop huwa wanatutania wabana pua. Kama game lingekuwa linaruhusu kweli tupige game, kweli tufanye muziki wa kweli mimi naamini ningekuwa namba moja Tanzania kuwa na muziki mzuri, kuwa na muziki ambao unaweza uka-sale hata nje kimataifa.” Ameeleza.
Amesema kwa sasa haoni kama kuna mabadiliko makubwa yaliyofanyika kwenye muziki kiasi cha kuufanya muziki alioufanya zamani kuwa ni muziki uliopitwa na wakati.
“Kilichobadilika sasa hivi labda ni temple ya muziki imebadilika, lakini pia fitina zilizopo kwenye muziki, kwa maana kwamba muziki sasa hivi lazima uwe na uwezo (kifedha) ili uweze kuufanya muziki wako vizuri. Lakini kwa uwezo wa uimbaji kusema ukweli mimi bado sijaona mtu yeyote anaenitishia amani Tanzania…samahani kwa kusema hivyo lakini..”
Katika hatua nyingine, akiwa katika kipindi cha Sun Rise, Mez B amesema baada ya kuachia wimbo wa ‘Shemeji’ ameamua kufanya kampeni ya kuhamasisha watu watulie katika ndoa zao na kuachana na michepuko na ataifanya katika mikoa 5 tofauti.
Ataendesha kampeni hiyo katika mikoa ya Dodoma, Mtwara, Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam