NEWS

24 Juni 2014

Haya ndio majibu ya Kitale 'Mkude Simba' kuhusu mahusiano yake na Vj Penny

Msanii wa filamu za vichekesho, Kitale, ambae kwa sasa anatambulika zaidi kwa jina la ‘Mkude Simba’ amekanusha kuwa hajawai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Vj Penny ambae aliwai kuwa mpenzi wa zamani wa Diamond.

 Kitale na Penny.


Kitale akizungumza Global TV hivi karibuni ,amekanusha uvumi huo, ambao uliambatana na picha ambazo zinaonyesha Penny wakati akimbusu Kitale.

“Penny mimi sina mahusiano nae yoyote, siyo kweli sina mahusiano nae , mimi nina ndoa yangu na nina mke wangu na nina mtoto, naiheshimu ndoa yangu”Alisema Kitale.

Penny na Kitale