Mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Subrina Rupia ‘Cathy’
Akizungumzia kuhusiana na kuwepo kwa madai ya wasanii wa kike Bongo Movie kujiuza, Cathy alisema hawezi kuweka wazi kama anawajua wahusika au la, isipokuwa tatizo lipo kwa wasanii wa kiume wenye majina ambao hukutana na mademu popote na kuwalazimisha wacheze filamu kutokana na masilahi yao binafsi.
“Penye ukweli lazima tuongee maana sisi zamani haikuwa hivi, msanii anapikwa kambini ndiyo baadaye anapewa nafasi ya kuonekana,
sasa siku hizi sivyo, mfano siku moja tulikuwa maeneo ya uwanja wa ndege kuna mdada akapita ambaye kiukweli muonekano wake siyo kabisa, cha ajabu kuna msanii wa kiume mkubwa tulikuwa naye akamshobokea na kumlazimisha acheze filamu yake,” alisema Cathy pasipo kutaja jina la msanii huyo.