NEWS

9 Septemba 2014

Anti Lulu Asema Mazito 'Nataka Kuzaa na Diamond Platnumz' 'Pata Michazpo zaidi'

MOYO unahifadhi mengi! Msichana wa mjini asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ amefunguka kwamba yupo tayari kuzaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwani amepata taarifa kwamba anasaka mtoto lakini wanawake anaokuwa nao hawataki kumzalia, Ijumaa Wikienda linakupasha.



BILA KUMUNG’UNYA MANENO
Akizungumza na gazeti hili bora la mastaa Bongo akiwa dukani kwake Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita, Anti Lulu bila kumung’unya maneno, alifunguka kwamba hivi karibuni alifuatwa na ndugu wa karibu wa Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita na kumuomba afanye jitihada azae naye.

MAKUBWA!
Alidai aliambiwa kuwa kila Diamond akimpa kibendi mwanamke, huwa mwanamke huyo anakwenda kukitoa bila hata ridhaa yake (Diamond).

“Ndugu wa Diamond alinifuata hapa dukani kwangu akanitaka nizae na Dangote kwani anasaka sana mtoto na kila akimpa mwanamke mimba huwa anaichoropoa bila kuafikiana naye.“Sababu kubwa ya wanawake hao kutoa mimba ni kutokana na mpenzi wa Diamond ambaye ni Wema (Isaac Sepetu) kudaiwa kuloga ili mwanamke yeyote asizae naye na kila akimpa mimba mwanamke inatoka au anakwenda kutoa mwenyewe bila sababu yoyote,” alisema Anti Lulu.

Pamoja na tetesi hizo, Anti Lulu alisema haogopi lolote kwani amejizatiti ndiyo maana amejitokeza hadharani na kutaka kuzaa na Diamond.