NEWS

14 Septemba 2014

Hivi ndivyo Myweather alivyomdunda Madina kwa mara ya pili bila huruma

Floyd Mayweather Jr. amemdunda kwa mara nyingine tena bondia wa Argentina, Marcos Maidana katika pambano lililofanyika Alfajiri ya leo jijini Las Vegas.



Mayweather ameshinda kwa pointi. Wawili hao walizichapa kwa mara ya kwanza May 4, na Mayweather kushinda kwa pointi pia. Mayweather alikuwa akitetea mikanda yake ya World Boxing Association na World Boxing Council.




Mechi hiyo ya raundi 12 imefanyika kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden Arena jijini Las Vegas. Hata hivyo Mayweather ambaye ameingiza dola milioni 32 kwenye pambano hilo, amedai kuwa Maidana alimng’ata katika raundi ya 8.

Mayweather ameingiza zaidi ya dola 100 kwa mwaka huu peke yake kutokana na mapambano yake.