NEWS

6 Juni 2017

Je, Wanawake Mnaijua Hii Kazi Nyingine ya Limao? Jifunze Hapa..!!!


Moja ya mambo ambayo huchanga kuharibu afya ya nywele ni pamoja na tatizo la mba ambalo huchangia pia mhusika kupata muwasho wa kichwa wa hapa na pale.

Sasa leo naomba nikupatie hii mbinu asili ambayo huweza kusaidia kumaliza haraka tatizo la mba

Tumia juisi ya limao

Namna ya kufanya utatakiwa kutafuta malimao mawili makubwa kisha kamua kwenye kikombe cha chai chenye maji. Kisha tumia maji hayo yenye mchanganyiko wa limao kwa kuweka kichwani na uchanganye vizuri kisha acha kwa dakika 5 hadi 10 kabla ya kuosha nywele zako.

Fanya zoezi hilo kutwa mara mwili ndani ya wiki mbili mfululuzo na utaona mabadiliko