NEWS

7 Juni 2017

MBUNGE COSATO CHUMI ATOA MSAADA WA AMBULANCE NYINGINE JIMBONI KWAKE

Na Fredy Mgunda,Mafinga

MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya kituo cha afya cha Igohole ya wilayani Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lilikabidhiwa kwa uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa kituo hicho katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Igohole, mjini Mafinga.

Akikabidhi msaada huo Chumi alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Uadilifu na uaminifu kwa serilikali ndio umetufanya tushirikiane vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”

Alisema gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.
MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi akizungumza na wananchi wa Igohole wakati kukadhi gari la kubebea wagonjwa ambalo amepewa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 
MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi sambamba na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga wakikata utepe wa gari la kubebea wangonjwa la kituocha afya cha Igohole
hawa ni baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa kupokea msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa lilotelewa na mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .