NEWS

28 Februari 2018

AFYA YA WASTARA MUNGU MKUBWA!

MUNGU mkubwa! Afya ya staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma ambaye yupo kwenye matibabu ya mguu katika Hospitali ya Saifee nchini India imeanza kutengamaa na hivi karibuni anatarajiwa kurejea Bongo.

 

Akizungumza na Za Motomoto News, Afisa Habari, Uenezi, Mahusiano na Umma wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni, Masoud Kaftany alisema kuwa, tayari Wastara ameshafanyiwa oparesheni ya mguu na sasa anafanya mazoezi ya hapa na pale kisha ndani ya wiki hii atarejea nchini.

 

“Wastara anaendelea vizuri kabisa kwa sasa anachofanyiwa ni mazoezi tu na atarejea ndani ya wiki hii ndiyo tunajiandaa kumpokea uwanja wa ndege, niombe tu ushirikiano kwa wasanii wenzetu kujitokeza maana itampa faraja sana,” alisema Kaftany.

The post AFYA YA WASTARA MUNGU MKUBWA! appeared first on Global Publishers.