NEWS

20 Februari 2018

MSHINDI WA SHINDANO LA DISNEY KUPAA MPAKA HONG KONG

Farida Lubanza akionyesha kuponi ya mshindi.

Mmoja wa wateja, Edward Laurent aliyechezesha droo na kupatikana kwa mshindi kama inavyoonekana.

Meneja Masoko wa GSM, FaridaRubanza akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.

 

Mshindi wa Shindano la Disney lililokuwa linaendeshwa na Kampuni ya GSM kupitia maduka yake ya GSM MALL, limefikia tamati ambapo, Consolata Mlebuzi, Mkazi wa Mbezi, Dar ameibuka mshindi katika droo ya mwisho iliyochezeshwa leo.

 

Akizungumza wakati wa uchezeshaji wa droo hiyo, Meneja Masoko wa GSM, Farida  Rubanza amesema mshindi huyo ataenda kula raha Hong Kong, China na kuongeza kwamba shindano hilo lililoendeshwa kwa muda wa miezi miwili, limeendeshwa kwa uwazi na kuzingatia vigezo vya bodi ya michezo ya kubahatisha kama ilivyofanyika.

 

Rubanza amewataka wateja wa maduka ya GSM kuendelea kutumia huduma zao kwa kuwa zina ubora na kuongeza kuwa wanatarajia kuanzisha mashindano mengine ya namna hiyo hivyo wakae mkao wa kula.

 

Mshindi huyo atawasili muda wowote kufahamishwa taratibu za safari yake ambapo kwa mujibu wa GSM, anatakiwa kusafiri yeye na familia yake yenye jumla ya watu wanne.

The post MSHINDI WA SHINDANO LA DISNEY KUPAA MPAKA HONG KONG appeared first on Global Publishers.