WATEJA wa Kampuni ya Simu za mkononi Airtel Tanzania wameendelea kujishindia zawadi mbali mbali kwenye promosheni inayoendelea ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti.
Kwenye droo ya leo ambayo imefanyika jijini Dar es Salaam, wateja ishirini wamejishindia simu mpya za smartphones pamoja na modem za kisasa huku wengine 3,000 wakijishindia 1GB bando ya intaneti.
Akiongea wakati wa droo hiyo, Meneja Uhusiano Jackson Mmbando Airtel Tanzania amesema kuwa kampuni ya Airtel bado inaendelea kutoa zawadi mbali mbali zikiwemo simu za smartphones pamoja na moden huku kila siku wateja 1,000 wakijishindia bando ya 1GB.
Mpaka sasa kuna zaidi ya wateja elfu ishirini ambao wamejishindia simu aina ya smartphones na modem huku wengine 14,000 wakishinda bando ya intaneti ya 1GB. Promosheni yetu ni kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu na kwa hivyo kuingia kwenye droo mteja haitaji kujisajili. Kila mtu anatika kufanya ni kununua bando ya intaneti kwa kupiga 149*99# kisha kuchangua 5 Yatosha Smatika Intaneti halafu nunua bando ya siku, wiki au ya mwezi na kuingia kwenye droo, alisema Mmbando.
Washindi wetu wamekuwa wakitoka sehemu mbali mbali hapa nchini. Kwa mfano washindi wa smartphones wametokea mikoa ya Mtwara, Zanzibar, Mwanza na wengine Dar es Salaam.
Promosheni hiyo ya siku 30 inatarajia kufikia tamati mwanzoni mwa mwezi ujao huku bando ya 30,000 GB zikiwa zimetolewa kwa wateja 1,000 kila siku.
The post Wateja wa Airtel wajishindia smartphone kwenye promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti appeared first on Global Publishers.