Dar es Salaam. Taxify, ambayo imejitanua katika utoaji wa huduma zake barani Ulaya na Afrika, leo imetambulisha huduma yake mpya ya ‘Taxify Bajaj’ ambayo ni App maalum kwa ajili ya Usafiri wa Bajaj huku wakiichagua Dar es salaam kuwa jiji la kwanza katika uzinduzi wa huduma hii.
Kupitia uzinduzi wa huduma hiyo, Taxify sasa imepiga hatua zaidi katika jitihada zake za kupunguza msongamamo jijini Dar es Salaam, mara baada ya uzinduzi wa App yake maalum kwa ajili ya usafiri wa teksi miezi miwili iliyopita.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Maendeleo Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki, Shivachi Muleji alisema, ‘Taxify Bajaj’ ni App mpya ya Taxify jijini Dar es Salaam ambayo inaunganisha watumiaji wa usafiri wa Bajaji na madereva ndani ya dakika chache.
“Tunafurahi sana kuanzisha huduma hii kwa mara ya kwanza kabisa jijini Dar es Salaam pia ni tumaini letu kuwa huduma hii itapokelewa vyema. Tunaamini kwamba huduma hii inaendana na utamaduni wa wakazi wa jiji hili na kwamba itatoa urahisi wa watu kuchagua usafiri anaoutaka kwa gharama nafuu pindi mtu anapotaka kufanya safari zake za mjini”
Bei ya Taxify Bajaj ni kama ifuatavyo: -Nauli halisi ni TZS 750, TZS 350 kwa Km, TZS 75 kwa dakika, wakati bei ya chini kabisa itakuwa ni TZS 2,000.
Programu ya Taxify inapatikana kwenye mifumo ya Android na iOS na ina sifa za kipekee kama kutumia ETA yako na rafiki au mpendwa wakati wa safari, ambapo itakuwezesha kufanya makadirio ya kukodisha kabla ya safari na pia kupata msaada wa huduma kwa wateja kutoka ndani ya programu.
Kwa upande wake, Meneja Mwendeshaji wa Teknolojia hiyo nchini Tanzania, Remmy Eseka alisema, programu yao ya teksi ambayo ilizinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam imepokelewa vizuri sana mpaka kufikia sasa, zaidi ya kampuni ilivyotarajia hivyo inawahakikishia watumiaji wa wake kuwa Taxify itaendelea kuwepo hapa nchini.
“Kama kampuni ya teknolojia, Taxify daima inaangalia njia ambazo inaweza kufanya ili kutoa ufumbuzi bora katika usafiri. Sisi daima tunaendelea kujibu haraka na kwa ufanisi mahitaji ya masoko mbalimbali ambako tunafanya kazi. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa mbele kwenye soko la ushindani na kuwa namba moja kuongoza katika masoko yetu yote, “alisema Eseka.
Usafiri wa Bajaj unekuwa maarufu sana katika miji mikubwa likiwemo jiji la Dar kwa sababu usafiri huu ni suluhisho kwenye njia zenye foleni zaidi kuliko magari.
Kuongezeka kwa matumizi ya usafiri huu, unazifanya kampuni mbalimbali za Kiteknolojia kama Taxify kuja na suluhisho na kuboresha huduma hii ili kuwafikia watu wengi zaidi ambao wanapenda aina hii ya usafiri.
***
Kuhusu Taxify
Taxify inafanya kazi katika nchi 20 Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati, na Amerika ya Kati. Ilianzishwa mwaka wa 2013 huko Tallinn, Estonia, ambako pia ndiko yalipo makao makuu. Huduma hii inayotolewa kimataifa ina timu ya wafanyakazi takribani zaidi ya 350. Agosti 2017, Taxify ilitangaza ushirikiano wa kimkakati na Didi Chuxing, inayoongoza ulimwenguni kwa utoaji wa huduma ya usafiri kwa njia ya simu. Chini ya ushirikiano huo, DiDi itawekeza na kushirikiana na Taxify kuunga mkono ukuaji zaidi na uvumbuzi zaidi.
TAXIFY YAZINDUA HUDUMA MPYA YA ‘TAXIFY BAJAJ’JIJINI DAR ES SALAAM
16 Februari 2018, Dar es Salaam. Taxify, ambayo imejitanua katika utoaji wa huduma zake barani Ulaya na Afrika, leo imetambulisha huduma yake mpya ya ‘Taxify Bajaj’ ambayo ni App maalum kwa ajili ya Usafiri wa Bajaj huku wakiichagua Dar es salaam kuwa jiji la kwanza katika uzinduzi wa huduma hii.
Kupitia uzinduzi wa huduma hiyo, Taxify sasa imepiga hatua zaidi katika jitihada zake za kupunguza msongamamo jijini Dar es Salaam, mara baada ya uzinduzi wa App yake maalum kwa ajili ya usafiri wa teksi miezi miwili iliyopita.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Maendeleo Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki, Shivachi Muleji alisema, ‘Taxify Bajaj’ ni App mpya ya Taxify jijini Dar es Salaam ambayo inaunganisha watumiaji wa usafiri wa Bajaji na madereva ndani ya dakika chache.
“Tunafurahi sana kuanzisha huduma hii kwa mara ya kwanza kabisa jijini Dar es Salaam pia ni tumaini letu kuwa huduma hii itapokelewa vyema. Tunaamini kwamba huduma hii inaendana na utamaduni wa wakazi wa jiji hili na kwamba itatoa urahisi wa watu kuchagua usafiri anaoutaka kwa gharama nafuu pindi mtu anapotaka kufanya safari zake za mjini”
Bei ya Taxify Bajaj ni kama ifuatavyo: -Nauli halisi ni TZS 750, TZS 350 kwa Km, TZS 75 kwa dakika, wakati bei ya chini kabisa itakuwa ni TZS 2,000.
Programu ya Taxify inapatikana kwenye mifumo ya Android na iOS na ina sifa za kipekee kama kutumia ETA yako na rafiki au mpendwa wakati wa safari, ambapo itakuwezesha kufanya makadirio ya kukodisha kabla ya safari na pia kupata msaada wa huduma kwa wateja kutoka ndani ya programu.
Kwa upande wake, Meneja Mwendeshaji wa Teknolojia hiyo nchini Tanzania, Remmy Eseka alisema, programu yao ya teksi ambayo ilizinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam imepokelewa vizuri sana mpaka kufikia sasa, zaidi ya kampuni ilivyotarajia hivyo inawahakikishia watumiaji wa wake kuwa Taxify itaendelea kuwepo hapa nchini.
“Kama kampuni ya teknolojia, Taxify daima inaangalia njia ambazo inaweza kufanya ili kutoa ufumbuzi bora katika usafiri. Sisi daima tunaendelea kujibu haraka na kwa ufanisi mahitaji ya masoko mbalimbali ambako tunafanya kazi. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa mbele kwenye soko la ushindani na kuwa namba moja kuongoza katika masoko yetu yote, “alisema Eseka.
Usafiri wa Bajaj unekuwa maarufu sana katika miji mikubwa likiwemo jiji la Dar kwa sababu usafiri huu ni suluhisho kwenye njia zenye foleni zaidi kuliko magari.
Kuongezeka kwa matumizi ya usafiri huu, unazifanya kampuni mbalimbali za Kiteknolojia kama Taxify kuja na suluhisho na kuboresha huduma hii ili kuwafikia watu wengi zaidi ambao wanapenda aina hii ya usafiri.
The post TAXIFY YAZINDUA HUDUMA MPYA YA ‘TAXIFY BAJAJ’ JIJINI DAR appeared first on Global Publishers.