NEWS

16 Agosti 2018

Alichoandika Msemaji Mkuu wa Serikali Baada ya Ubalozi wa Marekani Kudai Uchaguzi wa Marudio Buyungu Ulikuwa na Kasoro

JANA Ubalozi wa Marekani ulichapisha tamko lao kuhusu uchaguzi wa marudio uliomalizika August 12, katika Kata 79 na Jimbo la Buyungu ambapo Mbunge wake alifariki.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa uchaguzi huo uligubikwa na matukio ya fujo na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi.

Walitoa mfano kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kuwasajili baadhi ya wagombea wa upinzani.

Pia wameguswa na vitisho vilivyotolewa na Jeshi la Polisi kwa Wagombea na wanachama wa vyama vya upinzani ikiwemo pamoja na kukamatwa kwa wagombea na kuzuia mikutano ya kampeni.

Muda mfupi baada ya taarifa hiyo kusambaa Msemaji wa Serikali Dr. Hassan Abbas amesema Serikali inajiridhisha juu ya taarifa hiyo na watatoa tamko lao punde.

“Kuna taarifa inasambaa kuhusu kinachodaiwa ni taarifa ya ubalozi mmoja kuhusu masuala ya ndani ya nchi. Tunajiridhisha. Tutatoa tamko punde” Msemaji Mkuu wa Serikali