Dada wa Rais John Magufuli, Monica aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza amefariki dunia jana Augusti 19, 2018.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa kupitia akaunti zake za kijamii ameandika ujumbe ukiambatana na picha ya dada huyo wa Rais Magufuli akisema;
“Nasikitika kuwajulisha kuwa Dada wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia asubuhi leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu.
"Natoa pole kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Familia ya Mzee Joseph Magufuli, Ndugu, Jamaa na wote walioguswa na msiba huu.
"Raha ya milele umpe e Bwana na mwanga wa milele umuangazie, Marehemu Monica Jospeh Magufuli asterehe kwa amani, Amina,”.

Juzi Jumamosi, Rais Magufuli alifika hospitalini hapo kumjulia hali dada yake.