NEWS

20 Agosti 2018

"Diamond ni Mdogo Wangu na Atabaki kuwa Mdogo Wangu" Mr.Blue Afunguka


Msanii wa muda mrefu kidogo Mr .blue amefungua na kukanusha taarifa kuwa yeye na Diamond platinumz wamekuwa na bifu la muda mrefu kitu ambacho sio kweli kabisa.

Mr. blue anasema kuwa kumekuwa na dalili zinazoashiria kuwa wao wawili wanabifu lakini ukweli ni kwamba mabifu mengi ya wasanii yamekuwa yakitengenezwa katika mitandao ya kijamii na mashabiki na wala sio kitu kingine.

Hata hivyo ,Mr. blue anasema kuwa Diamond kwake atabaki kuwa mdogo wake  katika swala la muziki na amekuwa hana bifu ili wasanii wengine wanaomwamngalia wasione kama mfano mbaya kwao.

Diamond mimi na yeye hatujawahi kuwa na bifu la face to face lakini tu kuna vitu vilikuwa vinaashiria kuwa tuna bifu, lakini sasa wakati mwingine lazima tukae na tu-prove watu wrong  kuwaonyesha mashabiki kuwa jamani , diamond ni mdogo wangu na atabaki kuwa ni mdogo wangu.

mimi nitasimama hivyo kwa sababu kama nitakuwa namchukia diamond ntakuwa sina sapoti na wasanii wengine ambao wanachipukia au wasanii wanaotaka kuendelezea muziki wetu.