NEWS

20 Agosti 2018

Ray C Afunguka Kumzimikia Lulu Tangu Atoke Jela


Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amefunguka na kueleza jinsi anavyovutiwa na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Ray C amedai kuwa tangu Lulu atoke jela Miezi michache iliyopita amebadilika sana kwani amekuwa mtu wa kumuabudu Mungu na kuoekana akiwa kanisani tu.

Ray C amesema Lulu amemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua, kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa.

Aisee, nimemfuatilia sana Lulu tangu ameanza kupata matatizo ya kesi yake (ya mauaji ya bila kukusudia dhidi ya msanii Steven Kanumba) amebadirika sana. Sasa amekuwa mtu wa kumtukuza Mungu.

Yaani nikiwa namwangalia picha zake au video zake mitandaoni anazoimba nyimbo za dini mpaka machozi yananilenga, hadi fikra zinakuja maana sikumbuki mara ya mwisho lini niliingia kanisani.

Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali. Hakika nimejifunza kitu kutoka kwake, nawashauri watu wajirudi kwa kutubu kwa mwenyezi Mungu kutokana na makosa waliyofanya, wasisubiri hadi matatizo yawapate”.

Tangu Lulu atoke jela Miezi michache iliyopita baada ya kufungwa kwa Miezi kadhaa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba, Lulu amekuwa kimya hasa Kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana Makanisani tu.

LEAVE A REPLY