
- Muigizaji Jimmy Mafufu akiwa na mkewe Upendo Meja baada ya kufika kwenye Ukumbi wa Alfa.

- Mafufu na mkewe Upendo wakikata keki

- …Mafufu akimpiga busu la nguvu mkewe baada ya kumlisha keki.

- …Mafufu akizungumza mambo mbalimbali kuhusu mkewe, kufanikisha harusi hiyo na kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki waliomsaidia kufanikisha sherehe hiyo.

- Zamaradi Mketema (kushoto) ambaye ni meneja wa Mafufu, akiwa ukumbini hapo pamoja na waigizaji wenziye.

- Waigizaji wa Bongo Muvi wakimkabidhi Mafufu zawadi yao

- Jacqueline Wolper akizungumza jambo baada ya kuitwa mbele

- Wolper akimtunza Mafufu baada ya kuzungumza mawili matatu
Jana ilikuwa ni funika bovu kwenye sherehe ya ndoa ya muigizaji Jimmy Mafufu iliyofanyikia kwenye Ukumbi wa Alfa, Morocco jijini Dar, kwani mastaa mbalimbali waliibuka kumsapoti muigizaji mwenzao ambaye alikuwa anajitwalia jiko na kuacha historia baada ya wasanii wengi kumwagia manoti msanii huyo na wengine kumuahidi zawadi mbalimbali.
Mastaa waliofanikiwa kufika kwenye sherehe hiyo waliogozwa na Jacqueline Wolper, Steve Nyerere, Zamaradi Mketema na kaka yake Said Bwela, Weru Sengu, Odama, Yusuph Mlela, Baga, QBoy Msafi, Tausi, Asha Boko na wengine wengi.
The post HARUSI YA MAFUFU YAACHA HISTORIA BONGO MUVI (Picha +Video) appeared first on Global Publishers.