NEWS

15 Agosti 2018

MAJALIWA AZINDUA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi wakati alipowasili kwenye  eneo la uzinduzi wa Ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na  Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali  Jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Ofisi ya  Mwanansheria Mkuu wa Serikiali, Wakili Mkuu wa Serikali na  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka jijini Dodoma Agosti  15, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Devis Mwamfupe, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, Katibu Mkuu wa Wizara ya  Katiba na Sheria , Profesa Sifuni Mchome, Mkurugenzi wa Mshtaka, Biswalo Mganga na  kulia ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali,  Dkt. Ally Posi. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vitabu wakati alipotembelea maktaba ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  aliyoizindua jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa, Paramagamba Kabudi (kushoto), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde  (wapili kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. 

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshirki  katika  uzinduzi wa Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi baada ya kuzindua  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mshtaka  jijini Dodoma, Agosti  15, 2018. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa, Paramagamba Kabudi na kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Seriakli, Dkt. Adelardus Kilangi. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaaga washiriki wa uzinduzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka   baada ya kuzindua Ofisi hiyo jijini Dodoma, Agosti 15, 2018.  Wapili kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramnagamba Kabudi na kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde. 

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

The post MAJALIWA AZINDUA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JIJINI DODOMA appeared first on Global Publishers.