MAZISHI ya mama wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo yamefanyika leo katika kijiji cha Bupandwa Mhela Wilayani Sengerema yakihudhuria na maelfu ya wakazi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza.
Katika usia wake Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo amesema kuwa hakika ni pigo kwake na kwa familia kwa ujumla kwani ameondokewa na mtu mhimu katika maisha yake na mwenyezi mungu ampumzishe katika nyumba yake ya milele daima kwani atamkubuka siku zote za maisha yake na ataendelea kutenda yale yote aliyojifunza kutoka kwake.
Paroko wa Kanisa Katoliki Mwangika Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu, Padri Hilary Faraja, akiongoza ibada hiyo akiongoza ibada fupi ya kumuombea mama wa shigongo wakati wa mazishi.
Katika mazishi hayo viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wamejitokeza kuungana katika kumpumzisha katika nyumba yake ya milekle ambapo pia Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba ambaye pia ni Mbunge wa Buchosa kupitia CCM, mbunge wa zamani wa Nyamagana na aliyekuwa waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Lawrence Marsha wameshiriki mazishi hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo (wa kwanza kulia) akiwaongoza ndugu zake kuweka shada la maua kwenye kabuli ya mama yao.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdllah Mrisho (wa pili kushoto),Mhasibu Mkuu wa Global Gropup, Laurence Kabende akifuatiwa na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally wakiwaongoza wafanyakazi wa Global Group kuweka shada la maua kwenye kaburi la mama wa Shigongo.
Watoto wa kike wa marehemu, Asteria Kapela wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao mpendwa.
Dada wa marehemu Asteria Kapela wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa wao.
Ngugu wa karibu wa familia ya James Bukumbi wakiweka shada la maua.
Wajukuu wa kike wa Bi Asteria Kapela nao wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa wao.
Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tezeba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Buchosa naye akiweka shada la maua kwenye kaburi la mama wa Shigongo kijijini Bupandwamhela, Sengerema.
Baadhi ya wajukuu wa upapende wa kiume wakiweka shada la maua.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana, Laurence Masha (wa kwanza kulia) akiweka shada la maua.
Paroko wa Kanisa Katolikia Mwangika Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu, Padri Hilary Faraja, naye akiweka shada la maua.

The post MAMA WA SHIGONGO AZIKWA BUCHOSA SENGEREMA appeared first on Global Publishers.