Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemtumia rambirambi Rais John Magufuli kufuatia kifo cha dada yake, Monica.
Monica alifariki jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi.
Mbowe pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ameandika katika ukusara wake wa Twitter akisema:
“Kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na wana CHADEMA wote, natoa pole na salaam za rambirambi kwa Mh.Rais @MagufuliJPM kwa kufiwa na dada yake Monica Magufuli, Mungu awape faraja, na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi”
Mwanachama wa Chadema, aliyewahi kuwa waziri katika utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Lazaro Nyalandu ameandika katika twitter yake akisema:“Natoa POLE kwa Mh. Rais @MagufuliJP na familia yake kwa kufiwa na dada yake mpendwa, Monica Magufuli. Hakika, MAISHA yana thamani kubwa. MUNGU awafariji, na ampe dada yetu pumziko la milele mahali pema peponi, AMINA”