NEWS

15 Agosti 2018

Sallam SK Afunguka "Rich Mavoko Hakuna Kitu Hajarudisha Hata Robo WCB"


Meneja wa WCB, Sallam SK amefunguka kwa kudai kwamba pesa ambayo wamewekeza kwa msanii Rich Mavoko bado haijarudi huku akidai hata yeye hajui kitu ambacho kimemfanya muimbaji huyo kwenda kulalamika Basata.

Muimbaji huyo ambaye yupo chini ya WCB, wiki iliyopita alienda Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kulalamikia mkataba wake aliosaini na label hiyo kubwa ya muziki nchini Tanzania.

Akiongea na The Playlist ya Times FM Jumatano hii, Sallam SK amedai kwamba mpaka sasa pesa ambayo wamewekeza kwa muimbaji huyo katika project zilizotoka haijarudi hata robo. “Pesa ambayo tumekeza kwa Rich Mavoko haijarudi hata robo,” alisema Sallam.