WAS HINDI wa droo ya saba na droo ya nane wa Shindano la Tusua Maisha na Global linaloendeshwa na Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na Sokabet, wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao walizojishindia, Ijumaa ya Agosti 24, 2018 katika ofisi za Global Publishers, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Washindi wanaotarajiwa kukabidhiwa zawadi zao ni Jackson Bwire, msomaji kutoka Ukerewe, Mwanza na Said Katambo wa Nachingwea, Lindi, waliojishindia pikipiki, Nobert Benjamin wa Nyamagana , Mwanza na Boniface Malick wa Bunju A jijini Dar es Salaam waliojishindia dinner set.
Wengine ni Benard Kasembe wa Pugu Mwakanga aliyejishindia headphones za kisasa za Beats by Dre, Gasper Ndimbo, mkazi wa Miseko, Mkuranga na Ally Bakari, Mkazi wa Vikindu waliojishindia jezi.
Ili kuwa miongoni mwa washindi, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.
Itume namba maalumu inayoonekana juu ya kuponi kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kuponi au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukulia zawadi. Vigezo na masharti vinazingatiwa.
Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
The post Tusua Maisha na Global, Ni Mwendo wa Zawadi Dailee! appeared first on Global Publishers.