Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akiangalia utendaji kazi wa kitengo cha Tehama (IT) kinavyofanya kazi.
Mmoja wa madaktari wa hospiatali ya Amana (kulia) akimfafanulia jambo Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akimsikiliza mmoja wa wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata matibabu.
…Akiwa katika dirisha la kutolea dawa.
…Akiangalia dawa katika stoo.
…Akizungumza jambo na wanafunzi wa mazoezi katika hospitali hiyo.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza kuwa huduma za uzazi kwa wajawazito zitolewe bila malipo katika hospitali na vituo vya afya vya serikali.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa ziara yya kujua hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali za Rufaa Temeke, Amana na Mwananyamala leo jijini Dar es Salaam.
Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa wanawake wajawazito , watoto chini ya miaka 5 na wazee wasio na uwezo wanapata matibabu bure kulingana na sera ya Afya inavyosema.
Ndugulile amesema kuwa kila mtoa huduma anapaswa kuandika taarifa ya mgonjwa kabla na baada ya kumpa huduma katika kituo chake cha kazi.
Ndugulile amewataka watoa dawa katika hospitali na vituo vya afya kuandika majina asilia ya dawa na siyo yale ya kampuni pamoja na kufuata muongozo wa dawa uliyowekwa na Serikali.
“Marufuku watoa dawa kuwaandikia wagonjwa dawa na kwenda kununua nje ya kituo cha afya na badala yake dawa zote zitolewe katika hospitali au kituo cha afya kama zimeisha zinatakiwa kuagizwa kwa haraka na nauagiza uongozi wa Hospitali ya Amana kuwarudishia wagonjwa wa wodi ya watoto waliokwenda kununua dawa nje leo hii ” amesema Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Temeke Dkt. Amaan Malima amesema kuwa changamoto kubwa inayowakumba ni upungufu wa watumishi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana Dkt. Meshack Shimwela amesema kuwa anaomba radhi kwa tatizo hilo lililojitokeza kwani hakuna tabia kama hiyo hospitalini hapo na amehaidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
The post WAJAWAZITO WATAKIWA KUPATA HUDUMA ZA UZAZI BURE appeared first on Global Publishers.