Wanasheria wa Mbunge wa Kyaddondo Mashariki nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, wameitaka Tume ya Haki za Binadamu ya Uganda kuingilia suala la mbunge huyo ambaye hali yake inazidi kuwa mbaya katika Kambi ya Kijeshi ya Makindye ambako anashikiliwa.
Katika barua iliyotolewa Jumamosi iliyopita, Agosti 16,wanasheria hao, kupitia kampuni ya Lukwago and Company Advocates, wanataka tume hiyo kulilazimisha jeshi limwachie Bobi Wine ili apate matibabu kutokana na kuharibika kwa figo wakati wa mateso.
Pamoja na kuishukuru tume hiyo kwa kupanga wanasheria hao kuitembelea kambi hiyo ya kijeshi, wamesema ni muhimu mbunge huyo apatiwe matibabu ya haraka kwani anavuja damu puani na baadhi ya mbavu zake zimevunjika na hakuna tiba yoyote aliyopewa.
The post Wanasheria Wataka Bobi Wine Akatibiwe Figo Yake Iliyoharibika appeared first on Global Publishers.