NEWS

3 Agosti 2018

WASTARA AMSHUKURU RAIS MAGUFULI

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Msanii wa Filamu nchini Bi.Wastara Juma (kulia) alipofika ofisini kwake jana jijini Dodoma kwa ajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Serikali kwa ujumla kwa michango waliyotoa kufanikisha matibabu yake yaliyofanyika nchini India katika hospitali ya Saifee.

Msanii wa Filamu nchini, Wastara Juma (kulia) akitoa shukrani zake Kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe za kumshuruku  Rais wa Magufuli kwa msaada aliyoutoa kwake.

Waziri  Mwakyembe (kulia) akiwa katika picha ya pamoja msanii wa filamu nchini Bi.Wastara Juma (katikati) alipofika ofisini jana Jijini Dodoma .

Msanii wa Filamu Bongo, Wastara Juma jana amefika katika ofisi za Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe jijini Dodoma kumshuruku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa msaada aliyoutoa kwake kufanikisha matibabu yake ya mguu yaliyofanyika nchini India katika hospitali ya Saifee Februari mwaka huu ambapo alieleza kwa sasa afya yake imeimarika.

The post WASTARA AMSHUKURU RAIS MAGUFULI appeared first on Global Publishers.