
MTANGAZAJI wa Clouds Media, Soudy Brown na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Dar es Salaam kwa madai ya kuonekana mitandaoni wakirusha pesa na kuzikanyaga.
Inadaiwa wawili hao walikamatwa jana baada ya kupost video hiyo mitandaoni inayowaonekana watu wakicheza wimbo ‘Iokote’ wa Maua Sama huku wakiwa wanakanyaga pesa hizo.
Imeelezwa pia kwamba baada ya kukamatwa, wawili hao walipelekwa Polisi Kinondoni lakini leo jioni wameshahamishiwa Kituo Kikuu cha polisi dar es Salaam (Central) kwa mahojiano zaidi.
Aidha, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao.
The post Soudy Brown, Maua Sama Watiwa Mbaroni appeared first on Global Publishers.