NEWS

24 Septemba 2018

SOUDY BROWN, SHAFFIH DAUDA WATINGA KORTINI KININJA -VIDEO

WATANGAZAJI wa Clouds Media, SoudyBrown, Shaffih Dauda, Msanii Maua Sama, Mpiga Picha, MX, Mshereheshaji MC Luvanda na watuhumiwa wengine wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 24, 2018, kwa ajili kusomewa mashitaka yanayowakabili.

 

Washatakiwa hao walishuka kwenye karandinga la Jeshi la Polisi wakitokea Kituo Kikuu cha Polisi (Central) walikokuwa wameshikiliwa huku wakiwa wamevalia kininja kuficha nyuso zao.

 

Soudy Brown na Maua Sama wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za udhalilisha nembo ya taifa baada ya kusambaa clips za video zinazowaonyesha watu wakichezea pesa halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Watuhumiwa wengine wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kuchapisha maudhui kwenye mitandao ya kijamii wanayomiliki (Blogs na YouTube) bila kuwa na kibali kutoka Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

 

kesi yao ya maombi ya dhamana inatarajiwa kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi.

 

SHUHUDIA SOUDY NA WENZAKE WALIVYOTINGA KININJA

The post SOUDY BROWN, SHAFFIH DAUDA WATINGA KORTINI KININJA -VIDEO appeared first on Global Publishers.