NEWS

30 Novemba 2018

Jaji kaomba Nusu Saa Kuamua Hatima ya Dhamana ya Freeman Mbowe

Hatima ya usikilizwaji wa rufaa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko iwapo itaendelea kusikilizwa na Mahakama Kuu au la itajulikana baada ya muda mfupi ujao.

Hatima hiyo itajulikana baada ya Jaji Sam Rumanyima kutoa uamuzi wa maombi yaliyotolewa na upande wa mashtaka ukiiomba Mahakama hiyo isimamishe usikilizwaji wa rufaa hiyo kwa madai kuwa haina mamlaka hayo.

Jaji Rumanyika ameomba kutumia muda wa nusu saa kuandika uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili kuhusiana na uwepo rufaa ya Serikali katika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kukubali kuendelea na usikilizwaji.