NEWS

30 Novemba 2018

RAIS MAGUFULI, KENYATTA, MUSEVENI WAKUTANA ARUSHA – PICHAZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni pamoja na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta mara baada ya Kikao hicho cha 20 cha Wakuu wanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.

 

Rais Magufuli akiagana na Rais Museveni mara baada ya kikao hicho. 

 

Rais Magufuli akiagana na Rais Kenyatta.

 

Magufuli akiwa na Museveni na Kenyatta wakati wakielekea kwenye Kikao chao cha Ndani Ikulu jijini Arusha.

 

Rais Magufuli akizungungumza jambo katika kikao chao na Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kushoto ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika kikao kilichofanyika Ikulu jijini Arusha.

 

Rais Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kikao chao pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika Ikulu ndogo ya Arusha.

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

 

Picha na Ikulu

The post RAIS MAGUFULI, KENYATTA, MUSEVENI WAKUTANA ARUSHA – PICHAZ appeared first on Global Publishers.