NEWS

31 Desemba 2018

JE Unafahamu Laana ya Kutembea na Mume wa Mtu na Madhara Yake ?



Kutembea na mume wa mtu sio jambo zuri japo wanawake wengi wanaona ni kawaida bila kujua wanajilimbikizia laana itakayofanya maisha yao kuwa magumu mbeleni.

Machozi ya uchungu ya mwanamke mwenzio juu ya mume wake hayafutiki haraka.. Ni kama zigo la kinyesi mgongoni linavutiwa na inzi pekeake.

Huyo mwanaume unaemuona Leo ana mke, Pesa na mali na kuona ndo fursa kwako kumpata kwasababu anajua kujali na anapesa za kutosha kukugharamia.... Ukirudi nyuma miaka 10-15-20 mwanaume huyo huyo alikuwa kama huyu unae mkataa leo

Unaye muona hajui kuvaa.... Hana pesa za kutosha.. Hana mali kwahiyo hakufai.

Wanaume wengi wanaanzia chini... Jitihada za wake zao zinawafikisha walipo Leo. Heshimu jitihada hizo.

Heshimu siku walizofunga kwa ajili ya waume zao.
Heshimu machozi waliomlilia Mungu awafikishe walipo...
Heshimu muda na jasho walilolitoa kuhakikisha waume zao wanaonekana watu mbele za watu.

Muombe Mungu akupe wa kwako hata kama masikini mpate utajiri pamoja. Na wewe ubige magoti , ulie na kufunga.

Wanawake wengi wanalalamika hawaolewi au Wachumba wanawaacha bila sababu za msingi. Wanasahau zigo la kinyesi walilobeba mgongoni. Mwanamke piga magoti muombe Mungu akusamehe kwa kumliza mwanamke mwenzio.

Tuwaombee watoto wetu na kuwaonyesha njia iliyo bora. Kuwafundisha dini ili wawe na mahusiano mazuri na Mungu... wasikumbwe na laana hii.

Ewe mama elimisha watoto wako. Ewe dada elimisha wadogo zako.

Tukishirikiana kwa pamoja tutayafuta machozi ya wanawake .