MABINGWA watetezi wa Ligi ya wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League JKT Queens wamepania kufanikiwa kulitetea kombe lao msimu huu baada ya kuanza kwa ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Evergreen Queens.
Mchezo huo uliokuwa na msimsimko kwa kuwa ulikuwa ni wa ufunguzi ulifanyika katika uwanja wa Karume, ulikuwa ni wa ushindani mkubwa kwa kila timu kupania kupata pointi tatu muhimu.
Mabao ya JKT Queen yalifungwa na Fatuma Mustapha aliyefunga mabao 5, Stumai Abdallah aliyefunga mabao 2 na Asha Rashid alifunga mabao 2 na kukamilisha jumla ya mabao 9.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Cliford Ndimbo amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia msisimko wa Ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.
” Ushindani ni mkubwa na tunahitaji mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa hamasa wanawake hali itakayosaidia kuweza kuwapa hamasa zaidi wachezaji wakiwa uwanjani,” alisema Ndimbo.
The post JKT Queen walitaka kombe lao msimu huu appeared first on Global Publishers.