MABINGWA mara 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wanaufunga mwaka kibabe kutokana na kuweka rekodi ya kipekee msimu huu licha ya kupitia katika kipindi kigumu cha uchumi huku kila mchezaji akicheza kwa ushujaa kutafuta matokeo uwanjani.
Yanga mpaka sasa wana pointi 50 baada ya kucheza michezo 18 na kushinda 16, wakitoa sare michezo miwili, huku wakiwa bado hawajapoteza hata mechi moja.
Rekodi zinaonyesha kwamba, Yanga wanafunga mwaka wakiwa ni vinara katika kila idara kwa kuwa wana mabao ya kufunga 35 na kinara wa kupachika mabao ni mshambuliaji wao, Heritier Makambo mwenye mabao 11, akiwaacha mbali washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi wenye mabao saba.
Wanaofuatia ni Eliud Ambokile wa Mbeya City na Said Dilunga wenye mabao tisa. Katika mabao hayo 35, wafungaji ni mabeki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ (2), Kelvin Yondani (1) na Andrew Vincent ‘Dante’ (1). Viungo ni Feisal Salum ‘Fei Toto’ (2), Rafael Daud (2), Jaffary Mohamed (1), Deus Kaseke (1) na Mrisho Ngassa (4). Kwa washambuliaji ni Amissi Tambwe (5), Ibrahim Ajibu (5) na Makambo (11). Rekodi nyingine ni ile ya Ajibu kuongoza kwa pasi za mwisho ambapo kwa sasa amefikisha pasi 13.
STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA
The post Yanga yafunga Mwaka Kibabe, Yafikisha 50! appeared first on Global Publishers.