NEWS

31 Desemba 2018

Kagere Afunguka Kuhusu Ligi Kuu ya Bongo

Kagere Afunguka Kuhusu Ligi Kuu ya Bongo
MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere ambaye alikosekana kwenye kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida United kutokana na kusumbuliwa na majeraha, amewataka mashabiki wa Simba kutokuwa na hofu juu yake.

Kagere alipata majeraha hayo katika mchezo wa kimataifa waliocheza dhidi ya Nkana FC ya Zambia amesema kwa sasa anaendelea vizuri hivyo atarejea uwanjani muda wowote akipangwa.

Kagere amesema ushindani ni mkubwa ndani ya Ligi na kila mmoja anatafuta matokeo hivyo wataendelea kupambana kutafuta matokeo.

"Nilishindwa kuanza kucheza dhidi ya Singida United kwa kuwa bado sikuwa fiti kuanza kupambana ila kwa sasa nipo vizuri nipo tayari kwa ajili ya mapambano.

"Mashabiki natambua wanahitaji ushindi ila tumefanikiwa kupata kutokana na wachezaji kucheza kwa kushirikiana, bado kazi inaendelea ili kufikia malengo yetu muhimu sapoti yao," alisema Kagere.