NEWS

31 Desemba 2018

Mavazi Yamponza Zari

WABONGO sio watu wazuri! Siku chache baada ya zilipendwa wa Na­sibu Abdul ‘Dia­mond Platnumz’ kuposti picha akiwa kwenye mavazi ya kihasara, upepo mbaya umempuliza baada ya Wabongo kumshushia matusi mazito kisa picha hizo.

 

Zari alijikuta kwenye ‘kiti­moto’ hicho mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuposti kwa mara nyingine picha mbalim­bali zinazomuonesha akiwa kwenye mavazi ya kuogelea yanayoonesha mauongo yake nyeti pembeni ya bwawa la kuogelea (swim­ming pool).

Kwenye picha hizo, mrembo huyo wa Kiganda mwenye maskani yake Af­rika Kusini (Sauz), alioneka­na akiwa na wanawe huku katika baadhi ya picha akiwa na ‘wine’ kuonesha kwamba ameamua ‘kutafuna’ mai­sha ndipo ‘wataalamu’ wa kuchamba watu bila sababu walipoanza kumshambulia.

 

Kupitia maoni waliy­oweka kwenye picha hizo, walimnanga kwa kutumia maneno makali ambayo hayaandikiki gazetini hali ambayo ilimuibua Zari na kuposti kipande cha video kujibu mashambulizi na kwa sababu asilimia kubwa waliokuwa wakimchamba ni Wabongo, akaona naye bora awachambe kwa Lugha ya Kishwahili.

 

“Jamani nikitaka kuvaa swimming cost kwa swim­ming pool hiyo ni maisha yangu, ukitaka kuvaa dera hiyo ni maisha yako usini­pangie maisha vile mimi sikupangii maisha naomba tuheshimiane, samahani,” alisema Zari.

The post Mavazi Yamponza Zari appeared first on Global Publishers.