MSANII wa muziki wa kizazi kipya, African Princess maarufu kama, ‘Nandy’, ameonyesha zawadi ya nyumba aliyowajengea wazazi wake kwa mwaka 2018 ambayo iko jijini Dar es Salaam.
Kupitia akaunti yake ya Instagram ameweka kipande cha video na picha ambazo zinaonyesha nyumba hiyo na maelezo yanayosomeka, “Mungu wangu na Baba yangu najua nakukosea sana kama binadamu na kama kijana ila nikipiga goti unajua namaanisha kutoka moyoni mwangu na unajua hakuna ninayemtegemea zaidi yako… Asante kwa kunipa uvumilivu, unyenyekevu, katika maisha yangu hasa kipindi hiki cha mwaka 2018!! Asante kwa hii zawadi ndogo ya wazazi wangu najua hii ni ndoto ya kila kijana mwenye kutafuta!!! Ni kila ndoto ya mwanadamu yeyote duniani kuona wazazi wake wako na furaha na ndiyo baraka zenyewe” .
Aliendelea kwa kuchukua nafasi ya kutoa shukrani zake kwa kuandika, “Nashukuru media zote , blogs zote, ma producers wote, mapromoters wote, familia yangu ya THT, familia yangu ya clouds, management yangu, Team yangu, marafiki zangu, Baba yangu wa kiroho Mtumishi MWAMPOSA , na mafans wangu wote ,bila kusahau na hatters wote kwa kunipa nguvuu na supports kwa namna moja au nyingine uwepo wenu ndio mafanikio yangu……..
Nilijipa nguvu kabla sijapewa
Nilijipa moyo kabla sijapewa
Nilijiamini kabla ya kuaminika
Nilijikubali kabla ya kukubalika
Popote ulipo kijana mwenye ndoto yoyote ile jua inawezekana ukiweka nia ukikubali mazuri na mabaya yote yakufikie sababu ni daraja na nguzo ya mafanikio yako bila kusahau MUNGU ndiye kila kitu. Nawapenda