NEWS

1 Desemba 2018

Simba Yawafuata Mbabane Kitemi

MSAFARA wa watu zaidi ya 30 wakiwemo wachezaji 21, kesho Alfajiri unatarajiwa kuondoka kwenda Eswatini, huku John Bocco na Meddie Kagere wakitamba lazima washinde.

 

Mbabane Swallows itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Mavuso Sport Center. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar, Simba ilishinda mabao 4-1.

 

Hata hivyo, kabla ya Simba kuondoka kesho, tayari Simba ilimtuma mratibu wake, Abassi Ally kwenda kuweka mazingira sawa kabla ya timu kuwasili hiyo kesho Jumapili.

 

Mkuu wa Kitego cha Mawasiliano cha Simba, Haji Manara alisema, msafara huo utaondoka na Shirika la Ndege la Ethiopia na wanatarajiwa kufika siku hiyohiyo.

 

WACHEZAJI SIMBA WAAPA KUPAMBANA

Akizungumzia mechi hiyo, mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere alisema: “Tunahitaji kufanya vyema katika mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane ili tuweze kusonga mbele. Lengo letu ni kuona tunafanikiwa kusonga mbele katika michuano hii kwa kuwafunga wapinzani wetu katika mchezo wa marudiano.

 

“Mbabane ni timu nzuri hivyo itajiandaa kuona inafanikiwa kufanya vizuri, lakini naamini mwalimu atafanyia kazi makosa yaliyojitokeza ili kufanya vizuri katika mchezo huo.”

 

Kwa upande wake nahodha, John Bocco alisema: “Mchezo utakuwa mgumu, hivyo tuna kibarua mbele yetu tunahitaji kujipanga ili kuweza kufanya vizuri kwani wapinzani wetu tayari wameshatujua vizuri hivyo itakuwa kazi kubwa kwenye mchezo wa marudiano.”

HARMONIZE alivyompigia WOLPER magoti Stejini, MAUNO Kama yoteee!!

The post Simba Yawafuata Mbabane Kitemi appeared first on Global Publishers.