MWANAMITINDO Jane Ramoy ‘Sanchi’ ameibuka na kudai kuwa msic-hana amb-aye kwa sasa anatamba kwenye mitandao ya kijamii kutokana na umbo alilonalo, Jacqueline Obed ‘Posh’ hamsumbui kichwa kwa sababu hawezi kujilinganisha naye
Akizungumza na Showbiz, Sanchi alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakimfananisha na yeye lakini kiukweli anaona kama wanajidanganya kwa sababu yeye na Posh ni vitu viwili tofauti.
“Unajua kuna watu wanaweza kukurupuka na kukufananisha na mtu lakini hamfanani, Posh ni cha mtoto kwangu, mimi na yeye wapi na wapi jamani? Hajanikaribia hata chembe, yaani ni kama maji na mafuta,” alijigamba Sanchi.