NEWS

2 Januari 2019

Amber Rutty Aweka Wazi Changamoto Anazopitia Tangu Atoke Jela



Video vixen maarufu Muscat Abubakary maarufu kama Amber Rutty amefunguka na kuweka wazi magumu aliyokuwa anapitia tangu alipotoka jela Wiki chache zilizopita.

Kwenyr mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi kwa njia ya simu, Amber Rutty alisema maisha ya jela siyo mazuri ndiyo maana tangu atoke kwa dhamana amekuwa na matatizo ya kiafya na kisaikolojia.

Aliendelea kusema kuwa kwa sasa hajawa sawa kwa ajili ya kuelezea kiundani kuhusu alichojifunza huko jela kwani hali yake bado haijatengamaa akirudi katika hali yake ya kawaida ataeleza mengi lakini kifupi watu watambue kuwa jela siyo mahali pazuri hivyo wawe makini.

“Kiukweli tangu nimetoka jela nimekuwa nikiumwa sana, yaani afya yangu siyo nzuri ndiyo maana sijaweza hata kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na maswali yao wanayohitaji kujua kutoka kwangu. Pamoja na ukweli kuwa afya yangu siyo nzuri pia kisaikolojia siko sawa hivyo nikiwa vizuri ndiyo nitaongea mengi”.

Amber Rutty na mpenzi wake wanakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo kesi yao bado inaendelea kuunguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu sasa wako nje kwa dhamana.Kabla ya dhamana hiyo, wawili hao walisota katika Gereza la Segerea kwa siku 25.