NEWS

2 Januari 2019

Zari Afungukia Magumu Aliopitia 2018 na Kuupokea 2019

Mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amefunguka mwaka 2018 na kuupokea 2019.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari alisema kuwa mwaka 2017 alipitia katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mama yake mzazi pamoja na aliyekuwa mume wake, Ivan.

Lakini Pia Zari alieleza namna alivyoutumia mwaka 2018 katika kujenga na kuyarekebisha baadhi ya makosa yake na matatizo aliyopitia.  Anasema alijijenga zaidi baada ya kuondokewa na wapendwa wake hao wawili na kuahidi kuwa yuko tayari kwa mwaka 2019.

Mwaka 2019, niko tayari kwa mwanzo mpya… Katika maisha, sisi huumiza, tunafanya makosa, tunasamehe, tunaendelea. Lakini, zaidi ya yote tunajifunza. Asante 2018, bado nina pumua.   Asante, nishirikishe hadithi yako ya maisha kwa mwaka 2018“.

2017 i was shattered in ways i could never explain, 2 major deaths of my loved ones, infidelity and other things. 2018 was all about picking up my broken pieces and rebuilding. 2019 am simply ready for a new beginning…. In life, we hurt, we make mistakes, we forgive, we move on. But, most of all & through it all we learn. Thank You 2018, i still have my breath. #Grateful #Blessed #Thankful Share with me your life story of 2018…