NEWS

2 Januari 2019

Atumbukia Kisimani na Kufariki Dunia

Mtu mmoja aitwaye Mikidadi Abdi mkazi wa Manyoni mkoani Singida amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima katika kitongoji cha Majengo wilayani Manyoni mkoani Singida.

 

Akizungumzia tukio hilo kwa simanzi kubwa, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo, Silvester Msogoti amesema kuwa majirani walisikia kishindo usiku wa saa tano  cha kitu kutumbukia kwenye maji.

 

Naye, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Dr. Kitundu Jackson amethibitisha kupokea mwili wa marehemu Mikidadi Abdi.

 

Mji wa Manyoni kutokana na kuwa na shida ya maji hasa nyakati za kiangazi, wananchi wengi wamekuwa na utaratibu wa kuchimba visima kwenye nyumba zao, jambo ambalo Idara inayo shughulikia Mazingira ya Halmashauri ya Manyoni huwataka wananchi kuhakikisha wanachukuwa tahadhari ya usalama.

The post Atumbukia Kisimani na Kufariki Dunia appeared first on Global Publishers.