NEWS

2 Januari 2019

ASLAY AGUSA HISIA ZA WENGI, AMKUMBUKA MAMA YAKE STEJINI! – VIDEO

Kila apandapo jukwaani au stejini kufanya shoo ni lazima utaburudika kwani uwezo wake wa kuimba kwa hisia humgusa kila atakayehudhuria kwenye shoo yake, lakini uvumilivu unamshindaga na kujikuta akiimba kwa huzuni unapofika tu muda wa kuimba wimbo wake wa ‘MAMA’ ambao humkumbusha kifo cha mama yake mzazi.

Anaitwa Aslay Isihaka, moja kati ya wasanii wenye umri mdogo lakini kipaji kikubwa, amefanya shoo ya kibabe sana usiku wa Januari mosi katika ukumbi wa Life Park Mwenge kwenye tamasha la Masauti Luxury.

Mbali na Aslay, wasanii wengine waliopafomu katika tamasha hilo ni pamoja na Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’, mkongwe wa muziki wa dansi, Christian Bella ‘Obama,’ Hamisa Mobeto, Hellen George ‘Ruby’ na Beka.

 

The post ASLAY AGUSA HISIA ZA WENGI, AMKUMBUKA MAMA YAKE STEJINI! – VIDEO appeared first on Global Publishers.