NEWS

1 Januari 2019

Hatukuwa na malengo mwaka 2018" - Mwinyi Zahera

Hatukuwa na malengo mwaka 2018" - Mwinyi Zahera
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa mwanzo wa msimu huu klabu yake ya Yanga haikuwa na malengo yoyote kutokana na kuwa na kikosi kidogo na kuwa na ukata.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari jijini Dar es salaam, Zahera amesema suala la Yanga kuongoza ligi mpaka sasa ni juhudi na mshikamano wa makocha, wachezaji na viongozi na kwamba mwanzo wa ligi, timu hiyo haikuwa na malengo yoyote.

"Tunaweza kusema kama wakati tulianza ligi hatukuwa na lengo lolote, tulijua timu ina matatizo na pia matatizo ya wachezaji. Tulisema tu kutokana na matatizo yetu, basi tucheze tu ligi na tuone itakavyokuwa," amesema Zahera.

Pia amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa mshikamano wao katika kipindi chote cha mzunguko wa kwanza wa ligi, akisema kwamba bila ya wao klabu isingeweza kufikia mafanikio hayo.

Yanga inatarajia kusafiri kuelekea Zanzibar kwaajiili ya michuano ya Mapinduzi inayoanza leo Januari mosi, ambapo Yanga iko katika kundi B pamoja na timu za KVZ, Malindi, Jamhuri, Azam na Yanga.