NEWS

2 Januari 2019

Mastaa wa Kike Waliyofanikisha 2018, Waliyopanga 2019!

Wema Sepetu

MWAKA 2018 umekwenda, huu ni mwaka mpya wa 2019! Asante Mungu kwa kutufanya tuwe kati ya wale waliojaaliwa kuuona tukiwa wazima. Kwa mastaa wa Bongo, wamepitia mengi kwa mwaka 2018, mazuri na mabaya. Wapo ambao hawataki hata kukumbuka yaliyowapata kwa mwaka huo lakini wapo ambao walitamani mwaka huo uendelee kuwepo kutokana na jinsi ulivyokuwa wa neema kwao. Katika makala haya baadhi ya mastaa wa kike Bongo wanaeleza waliyoyafanikisha kwa mwaka 2018 na waliyopanga kuyafanya 2019

IRENE UWOYA “MASHABIKI

zangu au watu wangu wa karibu wanaweza kuwa mashahidi katika hili, kila kukicha nilitamani sana mwaka huu kabla haujaisha nifanye kitu kizuri na cha historia ambacho nilikifanya siku ya bethidei yangu. Kingine ni kwamba nimeweza kumaliza ujenzi wa pub yangu ambayo itakuwa matata sana hivyo mwaka huu naona mambo yatakuwa mazuri zaidi

Kajala Masanja.

KAJALA MASANJA

“MIMI kwa kweli siwezi kukufuru Mungu kwa mwaka uliopita hata kidogo kwa sababu nimefanya mambo mengi. Kwanza nilipata kazi ambayo ninayo mpaka sasa na inafanya maisha yangu yanaenda vizuri. Kingine nimefanikiwa kupata ofisi yangu ambayo nitaizindua mwaka huu, kwa hiyo naona kabisa 2019 ni wa kufanya mambo makubwa zaidi. Kikubwa tuombeane uzima tu maana sisi tunapanga na Mungu naye anapanga.”

JACQUELINE WOLPER

“NILIKUWA na ndoto nyingi sana huko nyuma lakini zilikuwa zinatimia taratibu sana, mwaka uliopita ulikuwa ni mwaka wa kupanuka kimawazo zaidi na kukutana na watu mbalimbali nje na ndani ya nchi. Hivyo 2018 ulikuwa ni mwaka mzuri na matarajio yangu kwa mwaka huu wa 2019 ni kufanya mambo makubwa zaidi. Kwa kifupi niko siriasi sana na maisha yangu kwa hiyo napambana kila iitwayo leo.”
“MIMI jamani sijui nisemeje lakini kikubwa Mungu kanipa uhai, hiyo ndio muhimu zaidi na ninachomuomba tena anipe nguvu nyingine mwaka huu niweze kusonga mbele zaidi.”
“MWAKA uliopita ulikuwa ni mwaka mzuri sana na wenye mafanikio kwangu, siwezi kumkufuru Mungu. Nazidi kumuomba anisaidie niweze kusimama tena kwa mwaka huu mpya wa 2019.”

ZUWENA MOHAMMED ‘SHILOLE’

“JAMANI labda nikijisemea mimi watasema najifagilia lakini ukweli ni kwamba mwaka uliopita ulikuwa ni mzuri kwangu, yaani nilijifunza mambo mengi sana na nilifanikiwa zaidi katika biashara zangu. Pia niliimarika kindoa, sasa huko ninakoelekea naona ni kuzuri zaidi, nanichoomba Mungu anisimamie tu maana bila yeye, mimi siwezi.”

WEMA SEPETU

“MWAKA uliopita nilikutana na changamoto nyingi sana lakini zilikuwa ni za kunikumbusha natakiwa niweje kesho. Namshukuru Mungu changamoto hizo zimepita. Kubwa ambalo nimelifanya kwa mwaka wa 2018 ni kufungua duka langu la nguo za watoto. Ilikuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu, imetimia! Watu wamtarajie Wema mpya kabisa mwaka 2019.”

 

AUNT EZEKIEL

KWA kweli sidhani kama naweza kusema mwaka 2018 ulikuwa mbaya kwangu kwa sababu nilifanya vitu vingi na vyote vilifanikiwa. Nilipanga kufungua pub yangu, nimefanikiwa. Mwaka huu wa 2019 natarajia kufungua pub kubwa na duka la urembo. Kwa hiyo 2019 pia naamini utakuwa ni wa mafanikio makubwa kwangu maana nimejipanga vilivyo.”

JENNIFER KYAKA ‘ODAMA’

“KWANZA napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufika hapa nikiwa mzima kabisa. Mwaka uliopita kiukweli haukuniangusha hata kidogo, nilifanya vitu vyangu kimyakimya lakini vilikuwa ni vikubwa mno. Natumaini mwaka huu vitajulikana vyote na watu wataona jinsi 2018 ulivyokuwa wa mafanikio kwangu. Mungu azidi kutupigania ili mwaka huu uwe wa neema zaidi.”

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI

“MIMI jamani sijui nisemeje lakini kikubwa Mungu kanipa uhai, hiyo ndio muhimu zaidi na ninachomuomba tena anipe nguvu nyingine mwaka huu niweze kusonga mbele zaidi.”

 

 

The post Mastaa wa Kike Waliyofanikisha 2018, Waliyopanga 2019! appeared first on Global Publishers.