NEWS

2 Januari 2019

Ujumbe wa Mwaka Mpya Alioutoa Katiku Mkuu CHADEMA Dkt. Vicent Mashinji

Katibu Mkuu wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji amewataka  watanzania pamoja na dunia kujiandaa kuipokea serikali mpya chini ya chama anachokiongoza.
 
Dkt. Mashinji ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, akisisitiza wananchi kuielewa na kuipokea sera mbadala ya chama hicho.

"Pokeeni Sera Mbadala na jiandaeni kuipokea Serikali mpya inayoongozwa na CHADEMA baada ya October 25, 2020," amesema  Dkt. Mashinji.
Aidha kiongozi huyo ametoa ujumbe kwa watu wasiopenda siasa kwa kuwakumbusha kwamba siasa ni utaratibu mzima wa kufanya maaamuzi katika jamii hivyo waipende na wasiichukie.

"Wasiopenda siasa, waambieni hivi “siasa ni utaratibu mzima wa kufanya maamzi katika jamii au kundi fulani la watu ikiwemo familia, na pili, ni matumizi ya mamlaka katika kutekeleza maamzi hayo. Tafadhari Watanzania wenzangu tuipende, tuifanye na tuiishi Siasa" Dkt. Mashinji.