NEWS

1 Januari 2019

Wanne Watiwa Mbaroni na Mifuko 50 ya Simenti Iliyoibiwa Eneo la Ujenzi wa Majengo ya Serikali Dodoma

Jeshi la Polisi Jijini Dodoma  linawashikilia watu wanne kwa kudaiwa kuiba saruji mifuko 50 katika eneo la ujenzi wa majengo ya serikali Chamwino Ikulu mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, jiijini hapo jana.

Alisema watuhumiwa walikamatwa jana Disemba 31, 2018 wakiwa wamepakia mifuko hiyo ya saruji kwenye lori.

Kamanda Muroto alisema watuhumiwa wanasadikiwa kuvunja stoo na kufanikiwa kuiba mifuko hiyo 50 ya saruji kwa lengo la kwenda kuiuza.  Alisema upelelezi ukikamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani