NEWS

29 Aprili 2019

BREAKING: Wanachama NSSF Wakinukisha! Wafanyakazi Watimua! – Video

BAADHI ya wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wamekusanyika leo Jumatatu, Aprili 29, 2019 katika Ofisi za NSSF wilaya ya Kinondoni zilizopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakidai malipo ya stahiki zao.

Wakizungumza na Global TV nje ya ofisi hizo, kwa nyakati tofauti, wanachama hao wameilalamikia NSSF wakisema  imeshindwa kuwalipa mafao yao kwa wakati licha ya kukamilisha taratibu zote na kuahidiwa kulipwa, wamedai wamekuwa wakipoteza muda mrefu kufuatilia malipo yao bila mafanikio huku wakimuomba Rais John Magufuli kuingilia kati suala hilo.

Hata hivyo, baadhi ya wafanyakazi wa NSSF waliokuwepo, walijifungia ndani ya vyumba vya ofisi hiyo na kugoma kuzungumzia sakata hilo, huku jengo zima la ofisi zao likiwa giza.

Aidha, Meneja wa Mkoa wa NSSF amezungumza na Global TV kwa njia ya simu na kukiri kupokea malalamiko hayo na kuahidi kuwa yupo njiani anaeleka ofisini kwa ajili ya kutatua mgogoro huo na kwamba tatizo kubwa lililokuwepo ni kuharibika kwa miundombinu ya umeme kwa siku kadhaa hadi leo na kusababisha kushindwa kufanya kazi.

TAZAMA TUKIO HILO HAPA

The post BREAKING: Wanachama NSSF Wakinukisha! Wafanyakazi Watimua! – Video appeared first on Global Publishers.